jana wkati naangalia TBC Kwenye sherehe za
Mashujaa zilizoongo zwa na Rais nilipatwa na
masikitiko makubwa sana hasa nilipouona ule
Mnara wa MASHUJAA wa vita vya kagera
Niliwakumbuka sana wapiganaji wenzangu
waliopoteza maisha yao wakiwa mstari wa mbele
wa mapambano ya kuuondoa Utawala wa Nduli
Idd-Amin wa Uganda.
Niliwakumbuka askari 25 waliokufa wakiwa
kwenye platoon yangu niliwakumbka mmoja
baada ya mwingine na nilisema MASHUJAA
TULIORUDI TUMERUDI KISHUJAA NA MASHUJAA
WALIOKUFA WAMEKUFA KISHUJAA LENGO NA NIA
YETU ILIKUWA NI MOJA TU KUILINDA HADHI YETU
YAANI NCHI YETU.
Tarehe 28-10-1978 nilikuwa kambini LUGARO
kikosi cha MMJ nilikuwa nimejipumzisha ghafla
likapigwa Baragumu na tulipoenda kusikiliza
tuliambiwa kuwa kuwa Idd-Amin kavamia huko
Kagera tukaamliwa kuchukua vitu vyetu na
kuvipeleka kwa STORE-KEEP vikiwa na majina
mimi nilichukua bage langu na kuliandika jina
langu na kulikabidhi kwa STORE-KEEPER.Na hapo
hapo tulianza kuchukua vifaa vya kivita kama vile
Combat mpya Bunduki SMG ya kwangu ilikuwa
NHN 66482612.
Jioni hiyo ya 28-10-1978 Tulichukuliwa na magari
ya Jeshi kwenda station ya Railway huko Dar-es-
salaam na tuliondoka usiku huo huo kuelekea
station ya ISAKA-Kahama.
Tulifika Station ya Railway ya Isaka 01-01-11-1978
Mchana tulikuta mabasi mengi sana ya kiraia
yametusubiri kwenda Vitani mimi na wenzangu
tulipanda Basi moja lilikuwa limeandikwa
LUPONDIJE lilikuwa na namba MZA 234
Tuliondoka hapo isaka saa 9 mchana kuelekea
Kahama mjini bahati mbaya sana Basi letu
lilipofika tu pale stand ya Kahama Msafara wa
magari yote ndo ulipoanza kuondoka na sisi
ilibidi tupitilize tu bila kupata chakula hapo na
kwa kufupisha habari nilifika kwenye uwanja wa
Mapambano 03-11-1978 Mchana
Nilipofika wakati nateremka Kwenye Basi mimi
niliitwa naMajor mmoja kuwa nichukue askari
wanne niende kwenye Landrover ya Jeshi ilikuwa
imefunikwa na turubai na nilifanya hivyo
nilipofungua nilikutana na Maiti za askari wetu
watatu waliolipuliwa na Bomu la kutupwa ilibidi
tuzishushe Maiti hizo na mimi ilikuwa mara
yangu ya kwanza kubeba Maiti katika Maisha
yangu Kwangu mimi niliona kama ni Uchuro
kwangu kufika tu Mstari wa mbele na kukutana na
Maiti kwangu mimi ilinipa taabu sana.
VITA VILIPOANZA
Baada ya plani ya vita kukamilika ndipo majeshi
yalipojipanga katika Brigade nne zikiongozwa na
Brigadier Kiwelu, Brigadier Mayunga, Brigadier
Marwa, na Brigadier Walden.
Msimamo wa vita ulikuwa umepangwa vizuri sana
na ulikuwa na MAKAMANDA wafuatao-
1. Brigadier Marwa waliingia Uganda kwa kupitia
mpaka na Rwanda na Zaire.
2. Brigadier Kiwelu alielekea Mbarara,
3. Brigadier Marwa alielekea Masaka
4. Brigadier Walden aliingia Uganda pia kwa
kupitia Rwanda na kuelekea Kasese
5. Brigadier Mayunga yeye alibaki upande wa
Tanzania ambapo brigade yake iligawanya katika
makundi mawili, kundi moja liingia maeneo ya
Mtukula kutokea Rwanda, , wakati kundi jingine
lilibaki pale pale mto Kagera lakini likiwa na
mizinga mizito (BM-40) kiasi cha kuweza kurushia
makombora hayo moja kwa moja hadi askari wa
Amini waliokuwa pale Mutukula. Ilichukua muda
wa karibu wiki tatu kwa plani ya vita kukamilika
na majeshi yetu kujipanga vile.
KIPIGO TOKA MAJESHI YA AMIN Baada ya majeshi
ya Amin kuchukua eneo la Mutukula,
walipandisha bendera ya Uganda na kubomoa lile
daraja la mto Kagera. Brigadier Yusuf Himid
ambaye alikuwa Brigade Commander wa Kanda ya
Magharibi wakati huo alituma Battalion moja
kujaribu kuvuka mto ule kwa kutumia mitumbwi
wakati wa usiku kusudi wakapambane na
wavamizi wale. Hata hivyo wakati platoon za
kwanza kwanza zinaanza kutekeleza amri hiyo,
wakaonekana na majeshi ya Amin ambayo
yalikuwa yamejikita kilimani; Askari wetu wale
walimiminiwa mizinga ambayo ilisababisha
hasara kubwa kwa askari. ..bahati mbaya sana
tulipigwa sana na majeshi ya amin na kupelekea
Majeshi yetu kurudi nyuma kujijenga upya na
kupelekea lile daraja kuvunjwa conteravertially
Bahati nzuri mimi na wenzangu tulikuwa
tumewahi kuvuka kwenye hilo Daraja na
Tulipojijenga upya kazi ilianza na ilikuwa ngumu
sana maana ilikuwa ni masika Mvua zilikuwa
zinanyesha sana sana kwa sababu mimi na
wenzangu tulikuwa askari wa Miguu Infrantry
haikutupa taabu tuliendelea kusonga mbele
kitendo hicho cha kurudishwa nyuma
kilisababisha Brigedier Yusuph Hamid
kuondolewa mstari wa mbele hivyo Brigade ya
magharibi ikawekwa mikononi mwa Colonel
(wakati huo) Kotta ambaye legacy yake kama
kamanda shupavu pamoja na vijana aliopigana
nao bega kwa bega na wote wakiwemo
makamanda ,maafisa na askari waliokomboa
afrika ..kama mnavyojua role ya jeshi letu kivita
angola,msumbiji,namibia,comoro ets...kwa
waliopo na waliotangulia mbele za haki.....
baada ya kile kipigo bregedia Yusuph Hamid
aliondolewa from front line kama ilivyokawaida
ya war plans...maana kamanda aliyepigwa
hulazimika kupumzishwa kwanza ili atafakari wapi
wapi alikosea.
Pale Ngome, kamanda aliyepanga vita ile yote
alikuwa ni Colonel Lupogo Baada ya plani ya vita
kukamilika ndipo majeshi yalipojipanga katika
Brigade nne zikiongozwa na Brigadier Kiwelu,
Brigadier Mayunga, Brigadier Marwa, na Brigadier
Walden.
Kipindi hicho mimi nilikuwa na ki-radio kidogo
cha mfukoni niliweza kusikiliza Radio Ujeruman
na Radio nyingi tu kila zilipokuwa zinatangaza
kutadhimini uwezo wetu wa kivita na uwezo wa
Majeshi ya Amini ilionekana wazi kuwa Maeshi ya
Amini yalikuwa Bora na zana Bora kuliko zetu kwa
upande wa vifaru sisi tulikuwa na T 34 vya
kizamani sana na Uganda vifaru walikuwa navyo T
55 Kwa wakati huo walikuwa navyo Bora sana
kuliko sisi.Pia Amini alisikika kwenye vyombo vya
habari akishangilia kuwa jeshi lake limeweka
rekodi kwa kuteka Mtukula kwa muda wa dakika
25 tu.
VITA VYAANZA RASMI FRONTLINE Baada ya
mejeshi yetu kujipanga ndipo filimbi ilipopigwa
na Brigadier Kiwelu akarusha risasi ya kwanza
dhidi ya Barracks moja ya Amin iliyokuwa pale
Mbarara. Brigadier Marwa naye akawarushia
risasi (ya kuwambia kuwa kazi imeanza) wale
askari wa Amini walikuwa pale Mutukula.
Brigadier Mayunga naye akadonoa kidogo kutokea
Magharibi, harafu akatumia ujumbe mwingine wa
BM-40 kutokea Kagera. Askari hao wa Amin
waliokuwa pale Mutukula (Simba Battalion)
walipoona wanapata kipigo kutoka pande zote
wakaomba msaada kutoka Mbarara, hata hivyo
wakaambiwa kuwa ile Battalion ya Mbarara nayo
ilikuwa imeelemewa na kipigo cha Kiwelu, ndipo
wakaomba msaada utokee Entebbe. Ile Battalion
iliyoletwa kutokea Entebbe ikakutana na kizingiti
pale....itaendelea
No comments:
Post a Comment