Saturday, July 27, 2013

Njemba moja yang'atwa uume wake

NJEMBA mmoja ameonja joto ya jiwe na
kuhatarisha mchakato mzima wa kujiburudisha
na kiburudisho lafiki cha wanaume. Ni baada ya
nyoka kuuma uume wake wakati akijisaidia
chooni.
Hata hivyo nyoka huyo hakuwa na sumu hivyo
hakumletea madhara jamaa huyo mwenye umri
wa miaka 35 ambaye hakufahamika jina kutoka
mjini Haifa.
Madaktari wa Hospitali ya Rambam walikuwa
wakimtibu majeraha yake kutokana na maumivu
aliyokuwa nayo katika sehemu hiyo ya siri.
Akielezea mkasa huo jamaa huyo alisema akiwa
anajisaidia katika choo hicho ghafla akahisi
maumivu makali ambapo akiwa katika taharuki
alimuona mnyama akitambaa chini ya miguu
yake.
Madaktari waliomhudumia walisema kwa sasa
anaendelea vyema baada ya kupatiwa matibabu
hospitalini hapo ingawa bado anahisi maumivu
katika sehemu hizo.
Hata hivyo walisema bado kiungo hicho kitabakia
kuwa na alama kutokana na kuumwa huko.
¡°Mtu huyu ana bahati kwa kuwa nyoka aliyemuua
hakuwa na sumu na kama angekuwa na sumu
basi ingemsababishia hatari kubwa kwa vile
sehemu hiyo ya mwili ni nyeti,¡± alisema mmoja
wa madaktari.
Daktari huyo alisikika pia akisema endapo
angekuwa ameumwa na nyoka mwenye sumu kali
kama cobra hali ingeweza kuwa mbaya zaidi kwani
angeweza hata kupoteza maisha.

No comments:

Post a Comment