1. Idd Amini - Alipoivamia Tz.... Mwalimu alitamka tutampiga nduli!.. Na kweli Idd Amini
alipigwa hadit akaikimbia Uganda....
2. Kolimba - Alipotamka CCM imepoteza Dira na
Mwelekeo... Mwalimu alimwita Dodoma
akamuuliza nani kakutuma useme hivyo?!.. Ndio
ukawa mwisho wa Kolimba!..
3. Samweli Sitta - Alipokuwa kiongozi wa serikali
ya wanafunzi UDSM aliongoza mgomo wa
wanafunzi wenzake kudai siagi na maziwa!...
Mwalimu aliibuka pale chuoni akamuuliza
Samweli Samweli kwenu mnakunywa maziwa
kweli?!.. Akamwambia lala chini, akamcharaza
bakora na mgomo ukaishia hapo hapo!...
4. Abdul Jumbe! - Alipotaka serikali tatu!.. Nyerere
alimuuliza moja kujumlisha moja ni ngapi?!..
Jumbe akajibu ni mbili!.. Nyerere akamwambia
kama ni mbili mbona unataka serikali tatu?!.. Huo
ndio ukawa mwisho wa Abdul Jumbe kuwa Rais
wa Zanzibar!..
5. John Samwel Malecela - Ni baada ya taarifa
kuzagaa kuwa amebadili dini na jina ili apate
kuungwa mkono na nchi za kiislamu kugombea
Urais mwaka 1995!.. Nyerere alimwambia wee
John wewe umeenda Arabuni mara moja
umebadilisha jina sasa unaitwa Jumanne!.
Ukienda mara ya pili si utabadilisha kabila?!...
Huo ukawa mwisho wa ndoto zake kuwa Rais wa
Tz !...
6. Edward Lowassa - Alipokodi ndege binafsi
ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya
mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka
1995 alimpa lift JK!.. Nyerere alimuuliza mmekuja
na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la
Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!...
Natamani Nyerere angekuwepo sasa na mwaka
2015!!......
No comments:
Post a Comment