Wednesday, July 31, 2013

Inasemekana Wachaga wanafanya mtaji harusi za watoto wao


Jamani sasa hvi ukitaka kuoa jiandae kikamilifu
kwa sababu imekuwa ni mtaji na harambee kwa
familia ya mdada unayemuoa. Tena kama
unaenda kuoa Moshi ndo balaa na ujipange zaidi.
Sikashifu mtu jamani ila natoa mfano hai. Jamaa
yangu kaenda Marangu Moshi pale Mamba
Kisambo kwenda kuoa. Masharti aliyopewa ili
kukamilisha mahari aliambiwa aandae vitu
vifuatavyo ili aandaliwe na ndoa kabisa..
Vitu hivyo alivyoambiwa aandae ni; Salary slip ya
mwezi uliopita, leseni ya biashara, hati ya
nyumba, apeleke tv flat screen, rice cooker, seti
za vyombo vya jikoni, suti ya mzee, vitenge wax
doti 3, subwoofa, sofa, kitanda 6 by 6, mahari
milion 1, orodha ya ndugu zako atakaoish nao,
kabati ya vyombo, deck ya dvd na king'amuzi cha
tv.
Jamaa zangu mnaoenda kuoa Kilimanjaro
jipangeni kama mmewapenda wadada wa kule

No comments:

Post a Comment