Wednesday, August 7, 2013

DUDU BAYA ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUCHOMA MOTO NYUMBA YA MSANII MWENZAKE

ANII wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu
Baya’ ameswekwa rumande kwa kudaiwa kuchoma
nyumba ya baba wa msanii mwenzake ‘Geez
Mabovu’, Mashaka Mrisho.
Tukio hilo lilitokea Agosti 1, mwaka huu ambapo
mwenye nyumba sambamba na polisi
walimkamata Dudu Baya na mkewe Mariam kwa
madai ya kuchoma moto nyumba kwa makusudi
na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
“Mkewe alitupia mkaa wa moto katika sofa,
likashika moto kabla majirani hawajanisaidia
kuuzima. Baada ya kuwauliza kulikoni
wakanitishia maisha ndipo nikawapeleka
polisi na kupewa RB namba OB/RB/13485/2013
na kuja kumkamata,” alisema Mashaka.
Dudu Baya alipotafutwa na mwandishi wetu,
alikiri kukamatwa na kuwekwa sero kwa saa sita
kabla ya kuwekewa dhamana na shemeji yake
aliyemtaja kwa jina la Vero.
“Vyumba vyake na vyangu haviingiliani kabisa,
tumetenganishwa na ukuta hivyo shutuma zake
hazina ukweli dhidi yetu ila naamini uchunguzi
wa polisi ndiyo utatoa majibu,” alisema Dudu
baya

No comments:

Post a Comment