Wednesday, August 7, 2013

Makala: Kwanini wanasoka wa Tanzania hawatoki kimapenzi na celebrities wa kike?

ZUNGUKA kumbi zote za disko.
Hautamuona mwanasoka yoyote wa Tanzania
amemshika kiuno mwanamke maarufu (celebrity)
katika
fani yoyote maarufu kuanzia, filamu,
muziki hadi siasa. Na sio hao tu,
wanasoka wa Tanzania wanaishi
dunia tofauti na wanawake wenye
hadhi za juu (high Personalities female) Wakati
David Beckham akihangaika na Victoria Adams ,
Cristiano Ronaldo akihangaika na mwanamitindo
wa
Kirusi, Irina Shayk, hali ni tofauti kwa mwanasoka
wa Tanzania. Ni nadra
kwenda katika klabu ya usiku
(Nightclub) na kumkuta Nadir Haroub ‘Cannavaro’
akiwa katika mtoko na
Mwanamitindo Flavian Matata. Unajua
kwa nini? Baada ya kazi ni wakati wa… (Photo
credit: kikuyumoja) Kuna sababu nne kubwa.
Kwanza ni
umaskini unaowakabili. Hawapo
katika kiwango cha kushindana
kifedha na mastaa wa fani nyingine
ndani ya nchi. Wakati mwanamuziki
Diamond anaweza kuingiza sh 30 milioni kwa
shoo za mwezi mmoja,
inamchukua Mrisho Ngassa miaka miwili ya
kusaini mkataba mpya ndipo
apate fedha hizo.
Wema Sepetu hawezi kwenda kwa
Mrisho Ngassa. Atakimbilia kwa
Diamond kwa sababu anajua
wanaweza kuagiza chochote wanachojisikia katika
hoteli yoyote ya
hadhi ya nyota tano bila ya hofu. Mwanadamu
anayesubiri shilingi 30
milioni baada ya misimu miwili ana
tofauti kubwa na mwanadamu
anayesubiri shilingi 30 milioni baada
ya wiki tatu. Kwa Ulaya na
kwingineko, hali ni tofauti. Wanasoka wameingia
katika soko la ushindani
wa kimaisha na wasanii na mastaa
wengine kutokana na mapato
makubwa wanayotapata ndani ya fani
zao, na katika matangazo ya biashara. David
Beckham, Kanye West na Tom Cruise wote
wanaweza kununua nyumba katika mtaa mmoja
wa
Beverly Hills, ni wazi kwamba wote
wapo katika nafasi sawa ya kutoka
kimapenzi na Kim Kardashian bila ya kujali kama
Kanye West amemuwahi. Lakini pia sababu ya pili
ya msingi
inayowanyima fursa wanasoka wetu
ni makuzi waliyopitia ambayo
yamewanyima fursa katika elimu na
tabia ya kujiamini katika maisha yao.
Wengi wao wamekosa uwezo wa kujiamini,
kujitawala kifikra na
kujiamulia mambo kwa uhuru.
Utaongea nini mezani na mrembo
anayejiamini huku akinywa Savannah
yake taratibu.
Wakati pesa likiwa tatizo la kimsingi, bado upeo
wa fikra kichwani ni tatizo
jingine linalokusumbua ukikaa na
mrembo aliyemaliza chuo kikuu au
IFM miaka sita iliyopita. Unahitaji kuwa
zaidi ya Jerry Tegete. Zaidi ya mabao,
una nini mezani. Pesa au elimu? Zaidi ya yote
haya. Wanasoka wa
Tanzania wametoka Ghetto. Ni
wachache waliotokea katika familia
zinazoeleweka kwa sababu mchezo
wa soka bado unabakia na taswira
kuwa ni mchezo wa kihuni na ni watu wa hali ya
chini.
Zao linatoka katika picha hii iliyopo
kuhusu soka, lazima litamtoa
mwanasoka ambaye kichwa chake
kwa asilimia nyingi kinafikiria uhuni
na kushindwa kujiamini katika fursa zilizopo.
Mwanasoka aliyetoka katika
familia isiyoeleweka hawezi kujipa
hadhi sawa na ya kujiamini mbele ya
Mwanamitindo anayefanya kazi zake
London, Paris, Milan na kwingineko na
ambaye amelelewa katika familia njema. Mpaka
wanasoka wa Tanzania
watakapoanza kutoka nje ya mipaka
yao na kuelimika nadhani watajipa
nafasi nzuri ya kuanza kutoka
kimapenzi na celebrities wa kike. Ni
kwa sababu wakiwa nje watakuwa kama wako
darasani huku
wakielimika na kujiongezea uwezo
mkubwa wa kujiamini. Nje, wanasoka
wanafundishwa jinsi
ya kujiamini, jinsi ya kuongea, jinsi ya
kujitawala na jinsi ya kujipenda. Na
zaidi ya yote watalalia paundi nyingi
na Dola ambazo zitajikuta zikiongea
zaidi kuliko midomo yao!

No comments:

Post a Comment