Majibu kwa
maswali yoyote kuhusu suala la mchezaji
Shomari Kapombe aliye chini ya mwongozo
wangu. Nimeamua nifanye hivi baada ya kuona
magazeti ya Tanzania yakipotosha mambo
mbalimbali kuhusu kijana huyu, mimi mwenyewe
na nini mipango yake. Pia naelewa waTanzania
wanashauku ya kujua mchezaji anaendelea vipi.
Ni muhimu muelewe kwamba, kama siwezi kujibu
swali ni kwasababu aidha inabidi niwe
nimeshawataarifu Simba kwanza (kama wamiliki
wa mchezaji) au ni kwamba tu siwezi kujibu hilo
swali, na ikiwa hivyo nitatoa sababu.
Naomba pia muelewe kwamba mimi nimeishi
huku miaka mingi (Uholanzi na Uingereza),
nimecheza mpira na ninaelewa mahitaji yake,
kwahiyo nimejipanga vizuri sana kumweka
mchezaji yoyote yule katika mazingira mazuri ili
afanikiwe. Ninafanya kazi na watu wanaojua kazi
zao. Ninafanya yote haya nikiwa na ufahamu wa
vikwazo nilivyopitia mimi kutokana na kutokuwa
na mwongozo mzuri na kushindwa kufanikiwa
kama mcheza mpira katika ngazi za juu.
Ninatumia uzoefu wangu huo kuhakikisha
Tanzania inapiga hatua.
Inabidi tukubali kwamba, waTanzania wengi
tunapenda short-cut na kuharakisha mambo ili
tufanikiwe maishani. Mimi nipo kuhakikisha
tunafanya mambo kwa mwendo mzuri wenye
kujenga na si kulipua. Kwa watu waliokuwa
wanapakazia kijana ametumwa sembe, naomba
mujiheshimu. Mimi ni Mhandisi katika kampuni
kubwa tu na ninaridhika na ninachopata, sihitaji
short-cut na ninawahakikishieni mchezaji yoyote
ninayemchukua namweleza asikubali kutumika
kwa vitu vya kijinga namna hiyo.
Nawakaribisheni mtiririke na dukuduku zenu.
Ninachoweza kusema ni kwamba, kijana
ameshacheza mechi mbili (mechi ya kwanza siku
10 baada ya kufika hapa, na mechi ya pili
jumamosi iliyopita). Mechi ya kwanza alipewa
offer 2 tayari na mechi ya pili nasubiri feedback
kutoka scout wa Hispania aliyependezwa na
mchezaji. Kuhusu offer zilizopo, swali ni je, ili
tusonge mbele tunaangalia maendeleo ya
mchezaji na taifa la Tanzania au maendeleo ya
mchezaji na timu ya Simba au faida kwa Simba tu.
Karibuni,
Denis
P.S,
Nimeamua nije hapa kwasababu naona kuna watu
wanatoa habari magazetini ambazo sio za kweli na
zinanifanya mimi nionekane ni mbabaishaji.
Nimeongea mara moja tu na mwandishi Saleh
Ally wa Championi baada ya yeye kunipigia simu
(infact alinibeep, mi nikapiga simu nikakutana na
maswali)...yaani nimechajiwa mimi kwa interview
ambayo sikuomba.
Pili Mtangazaji mmoja wa redio ile ya Lady Jay
Dee alinipigia simu. Yule jamaa nilimwambia
asinirekodi lakini akafanya hivyo akarusha habari.
Alirusha habari kiuchochezi maana niliongea nae
dakika 11 lakini akachagua acheze kipande
kitakachomfaa yeye. Kama angeamua kucheza
interview yote, mngeona jinsi alivyo mnafiki.
Huyu ni mtu aliyeniahidi kunipatia video za
wachezaji mbalimbali ninaowafuatilia Tanzania.
Hakufanya hivyo. Alinipigia simu siku hiyo akiwa
hajui kwamba mimi ndio nilimwomba hizo video
miezi michache kabla.
Naomba pia niwaambie kwamba sijawahi kusema
kijana anaenda kucheza FC Twente wala sikutaja
timu yoyote ile wakati nawaomba Simba ruhusa
wala Taifa Stars. Lakini kijana kaonekana na
mascout wamemuona, na nimehakikisha
anaonekana sababu najua ninachofanya. Sina
haja ya kuongea na gazeti lolote sababu sitaki
hiyo publicity na kwasabu mimi ni mtendaji na si
muongeaji.
No comments:
Post a Comment