Wednesday, August 7, 2013

Mbunge Hamis Kigwangalla hatompa kurasin yake Lowassa 2015

Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangalla amesema
hawezi kumpa kura yake Waziri Mkuu wa zamani
na Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward
Lowassa endapo jina lake litajitokeza kama
mmoja ya wagombea urais, ni kauli ya
Kigwangalla akijibu swali aliloulizwa na
Mtangazaji Fina Mango katika kipindi cha
Makutano kuhusu vuguvugu la urais 2015
linaloendelea ndani ya CCM juu ya mgombea
urais ambapo Edward Lowassa ni kati ya
wanaotajwa sana kama wagombea hasa katika
mitandao ya kijamii.
“Sitompa kura Mheshimiwa Edward Lowassa kwa
sababu za msingi tu, kwamba ninakipenda chama
changu na nina hakika chama changu kikija na
mgombea kwenye uchaguzi mkuu 2015 ambaye
ana historia ya kuhusishwa na mambo machafu
kama yale ya Richmond, Dowans ambayo
unayasema, hapa tunaweza kupata tabu sana
kuomba kura kwa wananchi, lakini pia tutakuwa
tumewapa hoja wapinzani wetu ya kusema tunalea
ufisadi, tunaubembeleza ufisadi kwa mikono
miwili’ Kigwangalla
Kwenye sentensi nyingine Kigwangalla amesema
Tanzania aihitaji rais asiyeweza kusimamia ukweli
ambapo kuhusu ishu ya dowans amesema haoni
tatizo la mitambo hiyo isipokuwa uamuzi
uliotumika katika upatikanaji wake.
Kwenye hii interview, Kigwangalla alitangaza nia
ya kugombea urais mwaka 2025 na kusema 2015
anaona bado ni mapema kwake kwani anaamini
watanzania bado hawajamjua Hamis Kigwangalla
ni mtu wa aina gani.

No comments:

Post a Comment