Wednesday, August 7, 2013

Real Madrid yaiua Chelsea,Ronaldo awachoma viwili

KIUNGO Frank Lampard alicheza kwa mara ya
kwanza majira haya ya joto, lakini alishindwa
kumzuia Cristiano Ronaldo kuinyanyasa Chelsea
jana.
Kabla ya mechi hiyo na Real Madrid mjini Miami,
kiungo huyo mkongwe alikosa mechi zote za
kujiandaa na msimu za klabu, Stamford Bridge
kutokana na kuwa majeruhi.
Lakini Lampard ameimarika na kuanza kazi tayari
kwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Hull
City, Agosti 18 baada ya kumaliza dakika 45 za
kwanza katika Fainali ya Mabingwa wa Kimataifa
wa Guinness.
Katika mechi hiyo, mabao mawili ya Ronaldo na
moja Marcelo, yalitosha kuitotesha timu ya Jose
Mourinho 3-1 dhidi ya timu yake ya zamani
ambayo kwa sasa inafundishwa na Carlo
Ancelotii.
Chelsea ilipata bao lake pekee kupitia kwa
Ramires.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas,
Arbeloa, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric, Khedira,
Isco, Ozil, Ronaldo na Benzema.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Terry, Cahill, Cole,
Lampard, Van Ginkel, Ramires, Oscar, Hazard na
Lukaku

No comments:

Post a Comment